• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wasisitiza hadhi muhimu ya rais Xi Jinping wa China wakati wa majadiliano na wabunge wa taifa

    (GMT+08:00) 2018-03-06 10:01:56

    Viongozi wa China wanaohudhuria Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya bunge la umma la China, wamesisitiza hadhi muhimu ya rais Xi Jinping wa China.

    Viongozi hao waandamizi ni pamoja na Bw Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning na Zhao Leji ambao ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China CPC.

    Bw. Li Zhanshu aliposhiriki kwenye majadiliano ya wabunge kutoka Mkoa wa Jiangxi, alisisitiza umuhimu wa Kamati Kuu ya CPC yenye rais Xi kuwa kiini, katika kuongoza maendeleo katika miaka mitano iliyopita.

    Alisema ni muhimu kutekeleza kikamilifu mawazo ya Rais Xi, hususan ya kiuchumi ambayo yanafuata mtizamo mpya wa maendeleo, na moyo wa Mkutano mkuu wa awamu ya 19 ya CPC ili kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako