• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaanza kurekebisha katiba kwa mara ya kwanza katika miaka 14 iliyopita

    (GMT+08:00) 2018-03-06 10:02:41

    Mswada wa marekebisho ya katiba ya China umewasilishwa kwenye bunge la umma la China, na yanatarajiwa kujumuisha kwenye katiba ya nchi fikra za rais Xi Jinping wa China kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.

    Naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya awamu ya 12 ya bunge la umma la China Bw. Wang Chen amesema, marekebisho hayo ya katiba ni hatua kubwa kwa China kuendeleza utawala wa kisheria na kuboresha mfumo na uwezo wa utawala wa China.

    Mswada huo unapendekeza kuweka fikra za rais Xi sambamba na fikra za Umarx-Ulenin, na Mao Zedong, nadharia ya Deng Xiaoping kuwa nadharia mpya ya kuongoza nchi kwenye katiba. Aidha mtazamo wa kujiendeleza kwa njia ya kisayansi pia umependekezwa kuandikwa kwenye katiba ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako