• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuboresha uwekezaji wa kigeni

    (GMT+08:00) 2018-03-06 16:36:00

    Makamu mkuu wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Ning Jizhe amesema, China itachukua hatua kuongeza uwekezaji wa kigeni kwa mwaka huu.

    Akizungumza kando ya mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China, Bw. Ning amesema China italegeza zaidi upatikanaji wa soko, itachochea uwekezaji kwa kutoa huduma bora zaidi na kuvutia mitaji ya kigeni kwenye mikoa mingi zaidi.

    Bw. Ning amesema, China itahakikisha ushindani wa haki kati ya makampuni ya ndani na nje ya nchi, huku hakimiliki ya ubunifu ikilindwa zaidi. Ameongeza kuwa sera chanya zinazohusiana na uhamishaji wa mitaji na matumizi ya ardhi inayonufaisha wawekezaji wa ndani pia zitatolewa kwa kampuni za kigeni zitakapowekeza katika mikoa ya kati, magharibi na kaskazini mashariki mwa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako