• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malengo ya ukuaji wa uchumi yaliyowekwa mwaka huu yameonesha matakwa ya kutafuta maendeleo yenye sifa nzuri

    (GMT+08:00) 2018-03-06 16:40:24

    Mwandaaji mkuu wa Ripoti ya Utendaji wa Serikali ya China Bw. Huang Shouhong amesema kuweka lengo la ongezeko la asilimia 6.5 la uchumi kwa mwaka huu, kumeonesha matakwa ya maendeleo yenye sifa nzuri. Amesema hatari za mambo ya kifedha zilizopo nchini China zinaweza kudhibitiwa kwa ujumla, na baadaye serikali itatunga sera ya kuzifanya serikali za mitaa ziwajibike daima.

    Ripoti ya Utendaji wa Serikali iliyowasilishwa jana kwa ajili ya kujadiliwa kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China, imesema mwaka huu pato la taifa la China linapangwa kuongezeka kwa asilimia 6.5, kiwango cha faharisi ya bei ya bidhaa CPI kitapanda kwa asilimia 3; idadi ya nafasi mpya za ajira mijini itaongezeka kwa milioni 11 na zaidi, kiwango cha matumizi ya sera ya jumla kitadumisha utulivu na hatari mbalimbali zinaweza kudhibitiwa kwa utaratibu na ufanisi. Akichambua ripoti hiyo, Bw. Huang Shouhong amesema mwaka huu malengo yote ya uchumi yameonesha matakwa ya kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri. Anasema,

    "Kwa nini mwaka huu tumeweka makadirio ya asilimia 6.5, sababu ni kuwa maendeleo ya uchumi wa China yamefikia kwenye kipindi cha kutafuta sifa nzuri kutoka kipindi cha kutafuta kasi kubwa. Iwapo uchumi utaendelea katika kiwango mwafaka, nafasi za ajira, masuala yanayohusu zaidi maisha ya watu yanahakikishwa, kasi kubwa kidogo na ndogo kidogo ya uchumi sio hoja. Tunachofanya kwa sasa ni kuhimiza mageuzi, mabadiliko ya kimuundo na kuzuia kutokea kwa hatari."

    Bw. Huang Shouhong pia amedokeza kuwa hivi sasa hatari za mambo ya kifedha zilizopo nchini China zinaweza kudhibitiwa kwa ujumla, madeni yaliyobaki kwa serikali kuu na serikali za mitaa ni Yuan trilioni 13 na trilioni 16 mtawalia. Anasema,

    "Kiwango cha madeni, yaani madeni yaliyobaki kwa pato la GDP sasa ni asilimia 36, ambacho ni chini ya makundi ya kiuchumi yaliyoendelea na yale yaliyoibuka hivi karibuni, kwa hivyo hatari ya mambo ya madeni inaweza kudhibitiwa kwa ujumla."

    Hata hivyo, Bw. Huang pia amesema baadhi ya serikali za mitaa zimesababisha hatari kutokana na kukiuka sheria na kanuni kwa kuahidi kulipa madeni kwa kutumia fedha za bajeti. Amesema katika siku za baadaye, China itazuia serikali za mitaa kuongeza madeni na kutatua suala la madeni yaliyobaki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako