• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China si upande unaozisababishia nchi za Afrika madeni mengi

    (GMT+08:00) 2018-03-06 19:36:26

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, madeni yanayozikabili baadhi ya nchi za Afrika yanatokana na malimbikizo ya muda mrefu, siyo ya miaka ya hivi karibuni tu, na kwamba China si upande unaozisababishia nchi za Afrika madeni mengi .

    Geng Shuang amesema hayo baada ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kusema baadhi ya nchi za Afrika kusini mwa Sahara zilipata mikopo yenye riba nafuu kutoka nchi nyingine, ambayo nusu kati yao inatoka China. Mikopo hiyo yenye riba nafuu imezisababishia madeni mengi nchi hizo za Afrika.

    Bw. Geng Shuang amesema, kauli hiyo haiendani na hali halisi, kwani msaada wa kifedha wa China kwa nchi za Afrika unawekeza katika sekta za ujenzi wa miundo mbinu na uzalishaji, na umeboresha mazingira ya maendeleo ya uchumi wa Afrika, na kuzisaidia Afrika kuvutia uwekezaji wa nje na kuimarisha uwezo wa kujiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako