• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: Fursa zipo tele kwa utalii Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-03-06 19:58:16

    Uongozi wa Hifadhi ya Taifa Jozani - Ghuba ya Chwaka visiwani Zanziba umesema, bado kuna fursa nyingi za kuongeza aina za utalii kwenye eneo hilo ukiwemo wa michezo ya mbio ndefu na kuendeleha baiskeli kwenye msitu wa asili na kambi za watalii.

    Mkuu wa Hifadhi hiyo, Ally Ally Mwinyi amewaeleza waandishi wa habari kuwa, bado kuna fursa ya kuongeza mapato kutokana na utalii Zanzibar kwa kuongeza aina za utalii badala ya kutegemea zilizopo kwa muda mrefu sasa.

    Kwa mujibu wa Mwinyi, hifadhi hiyo katika Wilaya ya Kati mkoani Kusini Unguja ndiyo msitu mkubwa zaidi Zanzibar ukiwa na ukubwa wa hekta 5,000 na kwamba, inafanya kazi kwa ushirikiano wa menejimenti na wananchi.

    Kwenye hifadhi hiyo iliyopo kilomita 35 kutoka mjini Zanzibar, kuna utalii wa kimazingira na utafiti wa wanyama na miti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako