• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuwa na mtazamo wa haki kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-03-07 09:21:25

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inatarajia nchi nyingine zifanye mazuri zaidi kwa ajili maendeleo ya Afrika, na kuwa na mtizamo wa haki na wenye kuzingatia ukweli kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Bw. Geng amesema hayo akijibu shutuma za Marekani kuwa mikopo yenye riba ya chini inayotolewa na China na nchi nyingine kwa nchi za Afrika, imezifanya baadhi ya nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara kudidimia zaidi kutokana na madeni.

    Pia amesema madeni katika baadhi ya nchi za Afrika ni matokeo ya malimbikizo ya madeni ya muda mrefu, na si hali inayojitokeza ghalfa. Amesisitiza kuwa China sio mkopeshaji mkuu wa nchi za Afrika.

    Bw. Geng Shuang ameongeza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha maendeleo ya viwanda, nchi yoyote inahitaji uungaji mkono wa kifedha, na kwamba ni vigumu kwa nchi za Afrika kutimiza maendeleo ya viwanda bila uhakikisho wa fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako