• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yanga yajiwekea mazingira magumu kusonga mbele

  (GMT+08:00) 2018-03-07 09:43:53

  Mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers ya Botswana, umemalizika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa wenyeji kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1.

  Township Rollers ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kwanza mapema kabisa kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye.

  Yanga waliendelea kupambana ambapo katika dakika ya 30, mshambuliaji Obrey Chirwa aliweza kufunga bao la kusawazisha. Hadi mapumziko timu hizo zilifungana goli hizo. Kipindi cha pili, Sikela akafunga bao la pili kwa Rollers katika dakika ya 83.

  Kwa matokeo hayo, Yanga italazimika kushinda zaidi ya magoli mawili kwa bila nchini Botswana katika mchezo wa maruadiano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako