Ripoti ya kazi ya serikali iliyotolewa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwenye ufunguzi wa mkutano wa bunge la umma la China, inaendelea kujadiliwa bungeni. Wataalamu na wachambuzi wa nchi mbalimbali duniani, wanaona kuwa mafanikio yaliyopatikana nchini China katika miaka mitano iliyopita ni ya kufurahisha, na nchi nyingine duniani zinatarajia kunufaika zaidi na maendeleo ya China.
Profesa Ling Xingguang wa Chuo Kikuu cha Fukui cha Japan amesema, ripoti hiyo imetumia takwimu zenye ushawishi kufafanua wazi mafanikio ya kihistoria yaliyopatikana katika sekta ya uchumi, na mageuzi ya kihistoria yanayotokea nchini China.
Mhariri mkuu wa Gazeti la Bara la Amerika katika karne ya 21 la Argentina Bw. Louis Bilbao amesema, China imepata mafanikio makubwa katika miaka mitano iliyopita, huku ikitoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi nyingine na kutia nguvu na imani kwenye ufufukaji wa uchumi wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |