• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanasayansi wavumbua betri ya Li-ion inayoweza kutumiwa katika joto la nyuzi 70 sentigredi chini ya sifuri

  (GMT+08:00) 2018-03-07 10:07:40

  Wanasayansi wa China wamesanifu betri ya Li-ion inayoweza kutumiwa katika joto la nyuzi 70 sentigredi chini ya sifuri, ambayo inatazamiwa kutumiwa katika maeneo yenye baridi kali duniani na hata anga ya juu.

  Kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Fudan kinachoongozwa na Xia Yongyao kimetumia kemikali aina ya Ethyl Acetate inayoweza kupitisha umeme katika mazingira yenye baridi kali kuwa elektrolaiti, na kutumia kemikali za kikaboni za PTPAn na PNTCDA kuwa elektrodi mbili.

  Elektrolaiti ni kemikali inayozifanya ioni zitiririke kati ya elektrodi mbili za betri, lakini mabadiliko ya kikemikali kati ya elektrolaiti na elektrodi hayawezi kudumu katika mazingira yenye baridi kali.

  Uwezo wa betri ya zamani ya Li-ion katika joto la nyuzi 20 sentigredi chini ya sifuri unapungua na kuwa nusu tu, na uwezo huo umepungua hadi kuwa asilimia 12 tu ya hali ya kawaida katika joto la nyuzi 40 chini ya sifuri.

  Prof. Xia amesema, ikilinganishwa na betri ya zamani, malighafi za kutengeneza betri mpya ni rahisi kupata, ni zabei nafuu na hazichafui mazingira. Amekadiria kuwa gharama ya kutengeneza betri mpya ni theluthi moja ya ile ya betri ya jadi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako