• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuisaidia Somalia kujenga mfumo wa kisheria

  (GMT+08:00) 2018-03-07 10:24:19

  Mwanasheria mkuu wa Kenya Bw. Githu Muigai jana alipokutana na ujumbe wa Somalia unaofanya ziara nchini Kenya, alisema Kenya itaisaidia Somalia kuimarisha mfumo wake wa kisheria, ili kuisaidia kukabiliana na changamoto za kijamii na kisiasa.

  Bw. Muigai amesema Kenya itatoa taaluma ya ufundi kuisaidia Somalia kujenga upya mfumo wake wa sheria.

  Vilevile ameongoza kuwa hivi karibuni Kenya itaanza kutoa mafunzo kwa maofisa wa sheria wa Somalia ili kuongeza uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao kwa haki.

  Waziri wa sheria wa Somalia Bw. Hassan Hussein Haji aliongoza ujumbe uliofanya ziara ya siku mbili nchini Kenya, kwa lengo la kujifunza uzoefu wa Kenya katika kuimarisha mfumo wa kisheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako