• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndege ya mzigo ya jeshi la Russia yaanguka Syria

  (GMT+08:00) 2018-03-07 14:18:12

  Wizara ya ulinzi ya Russia imesema ndege moja ya mzigo ya jeshi la Russia aina ya An-26 ilianguka jana kwenye kituo cha jeshi la anga cha Khmeimim nchini Syria, na kusababisha vifo vya watu wote 32 waliokuwa kwenye ndege hiyo, wakiwemo wafanyakazi 6 na abiria 26. Kwa mujibu wa wizara hiyo, ndege hiyo ilianguka mita 500 kutoka barabara ya ndege wakati ikijaribu kutua kwenye kituo hicho. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wakati ajali inapotokea ndege hiyo haikushambuliwa, na chanzo cha ajali hiyo kinaweza kuwa hitilafu za kiufundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako