• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapata mafanikio makubwa katika kazi za kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2018-03-07 18:16:56

    Naibu mkuu wa kikundi cha uongozaji wa kusaidia kuondokana na umaskini na kujiendeleza kilicho chini ya Baraza la Serikali la China Bw. Liu Yongfu leo amesema, katika miaka mitano iliyopita, China imepata mafanikio makubwa zaidi katika historia yake ya kuondokana na umaskini kwa kupunguza watu maskini milioni 68.53.

    Bw. Liu Yongfu amesema, China imetenga fedha nyingi katika mapambano dhidi ya umaskini, na kuboresha miundombinu na huduma za umma ya sehemu zilizoko nyuma kimaendeleo. Vilevile, sekta zenye umaalumu wa kipekee za sehemu hizo pia zimeendelezwa, na mazingira ya kimaumbile yameboreshwa kidhahiri.

    Kwa mujibu wa lengo la China, hadi kufikia mwaka 2020 China itawasaidia watu maskini wote wa vijijini chini ya kigezo cha sasa kuondokana na umaskini. Bw. Liu Yongfu amesema, China ina imani ya kushinda mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako