• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China washiriki katika mjadala na ujumbe wa mikoa kwenye mkutano wa bunge

    (GMT+08:00) 2018-03-08 10:17:44

    Viongozi wa China wakiwemo rais Xi Jinping, waziri mkuu Bw. Li Keqiang, pamoja na wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Li Zhanshu, Bw. Wangyang, Bw. Wang Huning, Bw. Zhao Leji na Bw. Han Zheng, wameshiriki kwenye mjadala na wajumbe wa mikoa wanaohudhuria Mkutano wa bunge la umma la China NPC.

    Akishiriki kwenye mjadala wa ujumbe wa mkoa wa Guangdong, rais Xi Jinping amesisitiza kuwa maendeleo ni jukumu kuu, wataalamu ni raslimali muhimu, na uvumbuzi ni msukumo mkubwa. Pia amesisitiza kuwa anaunga mkono mswada kuhusu marekebisho ya katiba, na kusema kuwa huu ni uamuzi muhimu uliotolewa na kamati kuu ya chama cha CPC kutokana na mahitaji na mtizamo wa kimkakati wa kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa kichina katika zama mpya, na pia ni hatua muhimu ya China kuhimiza utawala wa kisheria, na kusukuma mbele mfumo na uwezo wa utawala wa nchi uwe kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako