Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema mwaka huu mambo ya diplomasia ya China yataweka mkazo katika kuanzisha mazingira mazuri zaidi kwa maendeleo ya China na kutoa mchango kwa maendeleo ya shughuli za binadamu katika zama mpya.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye kituo cha habari cha mkutano wa kwanza wa bunge la 13 la umma la China, Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa huu ni mwaka wa kwanza wa kutekeleza mawazo yaliyoamuliwa kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, diplomasia ya China ikiongozwa na Fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, itafanya kazi mpya na kuonesha sura mpya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |