Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipojibu swali kuhusu jinsi China itakavyoshikilia urafiki na Afrika, amesema China ni nguvu na rafiki mkubwa wa nchi za Afrika, China itashikilia kufuatilia mahitaji na maslahi ya Afrika, kuratibu masuala muhimu ya Afrika, kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali katika mambo ya usalama, na kuzisaidia nchi za Afrika kuinua uwezo wao wa kulinda amani na usalama wao.
Amesema mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hapa Beijing. Mkutano huo utatilia mkazo China na Afrika kujenga pamoja "Ukanda Mmmoja, Njia Moja", kujenga mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika, kuuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmmoja, Njia Moja" kushirikiana na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali, na kuufanya ushirikiano kati ya China na Afrika kupata maendeleo makubwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |