• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sera ya kidiplomasia ya nchi kubwa yahimiza maendeleo ya urafiki kati ya China na nchi nyingine

  (GMT+08:00) 2018-03-08 17:30:07

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, amekutana na waandishi wa habari mjini Beijing kuelezea utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ya China katika mwaka uliopita, na mipango ya mwaka huu ya utekelezaji wa sera hiyo.

  Kwenye mkutano mkubwa na waandishi wa habari kutoka kila pembe ya dunia, Waziri Wang amesema katika mwaka ulipita Rais Xi Jinping akiwa msanifu mkuu wa sera ya kidiplomasia ya nchi kubwa, alihusika moja kwa moja katika kupanga na kutekeleza diplomasia "makini" ya kiongozi wa nchi. Rais Xi alitembelea nchi 57, na mpaka sasa wakuu 110 wa nchi mbalimbali duniani.

  Ziara zake na za wakuu wa nchi waliotembelea China, sio tu zimeimarisha uelewa wa dunia kuhusu China, bali pia zimeimarisha sifa ya China na ushawishi wake duniani, na kuchangia kwenye utatuzi wa matatizo mengi

  Waziri Wang amesema katika mwaka huu, mbali na shughuli za kawaida za kidiplomasia, serikali ya China itaandaa baraza la BOAO la Asia litakalofanyika mwezi ujao katika kisiwa cha Hainan, kusini mwa China, ajenda kuu ikiwa ni mageuzi na kufungua mlango kwa nchi wanachama.

  China pia itaandaa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Vile vile kutakuwa na shughuli mbili kubwa zitakazozihusisha nchi za Afrika, ambazo ni mkutano wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi Septemba, na Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa yatakayofanyika mjini Shanghai mwezi Novemba. Mbali na mikutano hii, Waziri Wang ametaja shughuli nyingine kubwa kubwa ni pamoja na Rais Xi Jinping kuhudhuria mkutano wa kundi la nchi 20 nchini Argentina, mkutano wa viongozi wa uchumi wa nchi za Asia na Pacific APEC utakaofanyika nchini Guinea, na mkutano wa nchi za BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini.

  Wanahabari wengi wa Afrika wamefuatilia zaidi, maelezo ya waziri Wang kuhusu baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, kwa kuwa ametaja kwamba kazi ya muhimu katika mkutano huo, itakuwa ni kushughulikia mambo ya mpango wa "ukanda mmoja, njia moja" mpango ambao una miradi mbalimbali ya kuzinufaisha nchi za Afrika. Waziri Wang Yi amesisitiza kuwa nchi za Afrika zitapewa nafasi ya kutumia mkutano huo kutia nguvu mpya ya uhai kwenye uhusiano kati ya pande hizo mbili, ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi. Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa yatakayofanyika mjini Shanghai yametajwa kuwa yatoa fursa kwa nchi za Afrika kuonyesha bidhaa zao na kutafuta fursa kwenye soko la China.

  Akimnukuu Rais Xi Jinping, Bw Wang amesema urafiki kati ya China na nchi za Afrika utaendelea kuwa imara, na China haiwezi kuwasahau marafiki zake wa Afrika. China inatambua kuwa changamoto mkubwa kwa nchi za Afrika kwa sasa ni kulinda amani na usalama. Kutokana na mahitaji hayo Bw. Wang amesema China itashirikiana na nchi za Afrika kukabiliana na matishio ya usalama kama ugaidi, uharamia na majanga ya asili, na itahimiza ushiriki wake kwenye utatuzi wa migogoro

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako