• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema itaendelea kuisaidia Afrika kwa nyakati zote, itahimiza amani na mapatano baina ya pande mbalimbali za Afrika

  (GMT+08:00) 2018-03-08 19:24:12

  Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bwana Wang Yi amesema Serikali yake itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mataifa ya Afrika wa wakati wote bila kujali mabadiliko yoyote na nyakati, ili kufanikisha suala la maendeleo ya kiuchumi kwa pamoja na kuboresha maisha ya watu.

  Akiongea na waandishi wa habari mjini Beijing kuwa masuala yanayofuatiliwa na China ndiyo masuala yanayofuatiliwa na Afrika pia, vipaumbele vya Afrika ni vipaumbele vya China, nchini za Afrika zinakumbwa na changamoto zinazofanana, ikiwemo amani na usalama, na maendeleo ya kiuchumi.

  Kutokana na udugu wa China na Africa, China itaendeleza juhudi za kuhimiza amani na mapatano baina ya pande mbalimbali za Afrika, pia itadumisha ushirikiano baina ya mataifa, kanda na umoja wa Afrika kwa ujumla, na itasaidia kupambana na baadhi vikwazo ikiwemo ugaidi na majanga mbalimbali, na kuhakikisha amani na usalama wa ukanda wa Afrika ambao ni marafiki.

  Kuhusu suala mkutano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mjini Beijing mwezi Septemba mwaka huu, Bw. Wang Yi amesema hiyo ni fursa muhimu kwa pande zote kupitia maendeleo ya mkakati wa kunufaishana.

  Baada ya mkutano na waandhishi wa habari, Idhaa ya Kiswahili ya CRI ilizungumza na mwandishi wa habari mwandamizi kutoka Kenya, Jane Kabura ambaye ametoa maoni yake kuhusu mkutano huo wa waziri wa mambo ya nje wa China na waandishi wa habari, pamoja na maoni yake kuhusu FOCAC.

  JANE KABURA:

  "Ni mkutano mzuri ambao umechukua saa mbili, na kila mambo yamewekwa mezani, kwa hiyo hii ni fursa nzuri na imempatia waziri fursa kama anavyofanya kila mwaka, kuiambia dunia, sera ya mambo ya nje ya China.

  Focac inatoa fursa kwa ajili ya majadiliano kuhusu ushirikiano, kuona ni sekta gani ama maeneo gani yanafaa kufanya uwekezaji, mfano kilimo, masomo, vyombo vya habari, hivyo nashauri viongozi wa Afrika wakija waje na mpango ili wajaue wanafanya nini kwa ajili ya maendeleo ya wananchi"

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako