Mjumbe wa Bunge la Umma la China Bw. He Leizhong amesema asilimia inayochukuliwa na matumizi ya ulinzi ya China katika pato la taifa GDP ni ndogo ikilinganishwa na ile ya nchi nyingine.
Bw. He amesema hayo baada ya serikali ya China kutangaza kuongeza bajeti ya ulinzi wake kwa asilimia 8.1 kwa mwaka 2018 na kufikia dola za kimarekani bilioni 175. Amesema ongezeko hilo si kubwa.Anasema,
"Serikali ya China inapanga bajeti ya ulinzi kwa mujibu wa matakwa ya kulinda usalama, mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kulinda maslahi ya maendeleo na kuongeza ujenzi wa ulinzi wa taifa na jeshi. Pia inaangalia ni kiasi gani nguvu za kiuchumi za taifa zinaweza kutumika kutimiza matakwa hayo."
Bw. He ameongeza kuwa mbali na asilimia ndogo ya matumizi ya ulinzi ya China katika pato la taifa, matumizi hayo kwa mwanajeshi mmoja mmoja na mwananchi mmoja mmoja pia ni kidogo kuliko nchi nyingine.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |