• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha Taifa Stars chatajwa, watano wa Zanzibar Heroes waitwa

  (GMT+08:00) 2018-03-09 09:42:08

  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ameteua wachezaji 23 kwa ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya timu za Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mwezi huu, safari hii akimuacha kipa Peter Manyika wa Singida United na kumchukua kinda, Ramadhani Kabwili wa Yanga SC.

  Katika mkutano na waandishi wa habari jana makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mayanga amewaita kikosini wachezaji wote wanaocheza nje ya Tanzania, akiwemo Nahodha mshambuliaji Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako