• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Qinghai yachukua hatua halisi kuwahudumia wakazi wa mkoa huo

  (GMT+08:00) 2018-03-09 10:04:38

  Mjumbe wa bunge la umma la China na katibu wa Kamati ya chama cha CPC ya Mkoa wa Qinghai Bw. Wang Guosheng, amesema serikali inapaswa kuchukua hatua halisi kuwaondolea matatizo watu wa makabila mbalimbali, ili kuwahudumia wananchi kihalisi.

  Bw. Wang Guosheng amesema, mkoa wa Qinghai una makabila madogomadogo 55 ambayo idadi ya watu wake ni zaidi ya nusu ya wakazi wote mkoani humo. Licha ya kukabiliwa na upungufu wa fedha na shinikizo kubwa la matumizi, mkoa huo ulitumia zaidi ya asilimia 75 ya bajeti yake katika kuboresha maisha ya watu ikiwemo ujenzi wa barabara, nyumba za makazi, elimu, na matibabu, hatua ambazo zimehakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa hatua kwa hatua. Amesema kuwa katika miaka mitano iliyopita, hali ya nyumba za theluthi moja ya wakazi mkoani humo imeboreshwa, idadi ya watu maskini imepunguzwa kwa zaidi ya milioni 1, na watu laki 1.4 wameanza kujishughulisha na ulinzi wa mazingira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako