• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mimea ya kale ni chanzo muhimu cha udongo duniani

  (GMT+08:00) 2018-03-09 14:38:21

  Je, chanzo cha udongo duniani ni nini? Pengine unaweza kujibu upepo, mvua na barafu zilisababisha miamba kuvunjika na kubadilika kuwa udongo, lakini hivi karibuni watafiti wa Uingereza waligunduwa kuwa mimea ya kale kwenye nchi kavu huenda ndio chanzo muhimu ya udongo na mchanga duniani.

  Miamba aina ya shale na slate ambayo iliundwa na chembe ndogondogo za udongo na mchanga inaonekana katika sehemu nyingi duniani, lakini ni nadra kugunduliwa kwenye tabaka la dunia lenye historia zaidi ya miaka milioni 500. Kikundi cha watafiti cha Chuo Kikuu cha Cambridge kimechambua mabadiliko ya kiasi cha udongo uliolimbikizwa chini ya mito ya miaka bilioni 3.5 hadi milioni 300 iliyopita, na kugundua kuwa kutokana na kustawi kwa mimea ya kale kwenye nchi kavu, kiasi cha udongo kwenye nchi kavu kiliongezeka kwa kasi kubwa.

  Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka milioni 458 iliyopita, udongo ulichukua asilimia 1 tu ya vitu vilivyolimbikizwa chini ya mito, kiasi hiki kiliendelea kuongezeka katika miaka milioni 100 ifuatayo, na katika kipindi kati ya miaka milioni 359 hadi miaka milioni 299 iliyopita, kiasi cha udongo kilifikia asilimia 26. Watafiti wamesema kustawi kwa kuvumwani katika miaka milioni 500 iliyopita na kuzaliwa na kuenea kwa mimea ya ngazi ya juu yenye mizizi mirefu katika miaka milioni 430 iliyopita kumesababisha kiasi cha udongo duniani kuongezeka. Lakini watu bado hawajui jinsi mimea ilivyoharakisha kutokea kwa udongo, na walikisia kuwa kemikali inayotolewa na mimea huenda ni sababu moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako