• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufungua mlango zaidi katika sekta ya mambo ya fedha

    (GMT+08:00) 2018-03-09 16:44:47

    Gavana wa Benki Kuu ya China Bw. Zhou Xiaochuan leo hapa Beijing amesema China itafungua mlango zaidi katika sekta ya mambo ya fedha.

    Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mageuzi na maendeleo ya mambo ya fedha, Bw. Zhou amesema, baada ya China kuingia kwenye kipindi kipya cha maendeleo, inaweza kufungua mlango zaidi na kulegeza vigezo vya kuingia katika soko la China. Licha ya kuruhusu mashirika ya nchi za nje kuingia China kushughulikia mambo ya fedha, mashirika ya kifedha ya China pia yamekwenda nchi za nje.

    Naye naibu gavana wa Benki /Kuu ya China Bw. Yi Gang amesema, kufungua mlango zaidi katika soko la kifedha siyo tu kutalegeza usimamizi, kwani mashirika ya kifedha ya nchi za nje yanapoingia au kufanya kazi nchini China, pia yanapaswa kufuata sheria za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako