• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya China na Idara ya Uendeshaji mashtaka zawasilisha ripoti kubainisha kazi za mageuzi ya mfumo wa sheria za mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-03-09 19:17:16

    Jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya China Bw. Zhou Qiang na mwendesha mashitaka mkuu wa Idara Kuu ya Uendeshaji mashtaka ya China Bw. Cao Jianmin leo kwa nyakati tofauti wametoa ripoti za kazi.

    Ripoti hizo mbili zimekumbusha utendaji kazi wa mahakama kuu ya China na idara kuu ya uendeshaji mashtaka, na kutoa mapendekezo kwa kazi za sheria za mwaka 2018.

    Kwenye ripoti ya kazi ya Mahakama Kuu ya China, Bw. Zhou Qiang amesema jumla ya wafungwa 31,527 wamepewa msamaha nchini China katika miaka mitano iliyopita. Amesema kuwa, mahakama nchini China zimeimarisha juhudi za kulinda haki za binadamu katika shughuli zake, na kwamba hukumu za kifo zinafanyiwa tathimini ya kina ili kuhakikisha kuwa kuhumu hiyo inatolewa tu kwa idadi ndogo ya wahalifu kwa makosa makubwa sana.

    Nayo ripoti ya kazi ya Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China imeonyesha kuwa, idara hiyo imechunguza watu zaidi ya laki 2.5 wanaotumia vibaya madaraka yao na kufanya uhalifu, na kuokoa hasara ya kiuchumi dola za kimarekani bilioni 8.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako