• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya KCB ilipata faida ya shilingi bilioni 19.7 mwaka jana

  (GMT+08:00) 2018-03-09 19:31:45

  Benki ya KCB ya Kenya imetangaza faida ya shilingi bilioni 19.7 katika mwaka wa 2017 . Faida hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 3 ikilinganishwa na mwaka wa 2016 ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni 19.2. Aidha ripoti ya benki hiyo imeonyesha kuwa kiasi cha fedha kilichowekezwa katika benki ya KCB kilionbgezeka kwa asilimia 11 kutoka shilingi bilioni 448 mwaka wa 2016 hadi bilionbi 499 mwaka jana. Ripoti hiyo inaonesha kuwa idadi kubwa ya wateja wanatumia simu za mkononi kupata huduma za benki. Mkurugenzi mtendaji wa KCB Joshua Oigara amesema kufikia Disemba mwaka jana, KCB ilikuwa na wateja milioni 13 wanaotumia simu kupata huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi.Benki hiyo pia imeelezea matumaini kuwa biashara huenda ikastawi mwaka huu kutokana na ongezeko la wateja wanaojiunga na huduma za simu na kupanuka kwa miradi inayolenga vijana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako