Bunge la Umma la China limepitisha muswada wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo hii leo.
Wabunge wanaohudhuria mkutano wa bunge unaoendelea hapa Beijing wamekubaliana kuwa marekebisho hayo ambayo yanaendana na maudhui ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na wananchi, na pia yamepokelewa vizuri ndani na nje ya Chama, yana umuhimu wa kihistoria katika kuhakikisha ustawi na usalama wa kudumu kwa Chama na taifa la China.
Muswada wa marekebisho hayo uliwasilishwa kwenye kikao cha kwanza cha Bunge la 13 la China kwa ajili ya kujadiliwa jumatatu. Haya ni marekebisho ya kwanza ya sheria muhimu za nchi katika miaka 14 iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |