• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia nchi za Afrika kujenga uwezo wa kujiendeleza kwa kujitegemea

    (GMT+08:00) 2018-03-12 09:35:53

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw Qian Keming amesema China itazisaidia nchi za Afrika kujenga uwezo wa kujiendeleza kwa kujitegemea, ikiwa ni sehemu ya hatua mpya za kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.

    Akizungumza na wanahabari kando ya mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China, Bw Qian Keming amesema China itafanya juhudi kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza umaskini, kuongeza nafasi za ajira, kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu.

    Ameongeza kuwa China itachukua hatua mpya za kuimarisha ushirikiano kati yake na Afrika kwenye sekta za uchumi na biashara kulingana na mahitaji ya nchi za Afrika. Amesema China itatekeleza pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja sambamba na Ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika, pamoja na mikakati ya maendeleo ya nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako