• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuimarisha ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja"

  (GMT+08:00) 2018-03-12 09:52:52

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan amesema China itachukua hatua zaidi kukuza ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja", ikiwa ni kipaumbele cha kazi za wizara yake katika kipindi kijacho.

  Amesema China itazindua majukwaa mapya ya ushirikiano, yakiwa ni pamoja na Maonesho ya Kwanza ya kimataifa ya Uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya China, maeneo ya majaribio ya biashara huria, pamoja na maeneo ya maendeleo na ushirikiano.

  Bw. Zhong Shan amesisitiza kuwa miradi mikubwa ya uwekezaji na kutoa misaada kwa nchi za nje itapewa vipaumbele ili kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na matokeo chanya ya kiuchumi na kijamii, inajitokeza miongoni mwa miradi mingine, na kuchukuliwa kama "lulu kwenye Ukanda mmoja, Njia moja".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako