• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapendekezwa kuhimiza ushirikiano wa kupambana na umaskini kati ya nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2018-03-12 16:30:06

    Mjumbe wa Bunge la Umma la China Zhao Wanping amesema kuondoa umaskini ni changamoto inayoikabili dunia nzima, na nyingi zilizo katika "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni nchi na sehemu zinazoendelea, ambazo zinakabiliwa na tatizo la umaskini, kwa hivyo kuna kazi nyingi za kufanywa katika ushirikiano wa kupambana na umaskini chini ya mpango huo, ambao utainua uwezo wa nchi hizo kupunguza umaskini na kupata maendeleo kwa pamoja.

    Mjumbe Zhao Wanping ambaye pia ni naibu mkuu wa Taasisi ya Sayansi Kilimo ya Mkoa wa Anhui, anahudhuria mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China unaoendelea hapa Beijing. Amesema katika miaka mitano iliyopita, watu milioni 68.53 wameondokana na umaskini katika sehemu za vijijini nchini China, na kiwango cha umaskini kimepungua kutoka asilimia 10 ya mwishoni mwa mwaka 2012 hadi asilimia 3. Kwa mujibu wa mpango na malengo yaliyowekwa, watu wanaohesabiwa kuwa maskini kwa mujibu wa kiwango cha sasa cha umaskini katika sehemu za vijijini wote wataondokana na umaskini ifikapo mwaka 2020. Amesema China inapenda kubadilishana njia, teknolojia na uzoefu wake, na nchi nyingine katika kazi za kupunguza umaskini.

    "Uzoefu huo mzuri na fikra ya rais Xi Jinping wa China ya kufanya kazi zinazowalenga kwa usahihi na kusaidia watu kuondokana na umaskini, sio tu vinamilikiwa na taifa la China, pia vinastahili kuenezwa kwa nchi nyingine, ili kuchangia busara na nguvu za China kwenye kazi za kupunguza umaskini duniani."

    Safari hii mjumbe Zhao Wanping aliwasilisha mapendekezo bungeni juu ya jinsi nchi zilizo katika "Ukanda Mmoja na Njia Moja" zinavyoweza kushirikiana katika kupambana na umaskini. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuimarisha ubunifu wa ngazi ya juu katika ushirikiano wa kupunguza umaskini kati ya nchi hizo, kutafuta nguvu ya kiuchumi ambayo haijatumiwa ipasavyo katika sehemu za vijijini za nchi hizo, na kuongeza mawasiliano na ushirikiano katika teknolojia ya kilimo.

    "Kwa mfano Taasisi ya Sayansi Kilimo ya Mkoa wa Anhui imefanya utafiti na kusanifu aina moja ya mpunga ambao hauhitaji ufundi wa ngazi ya juu wa kilimo, na unafaa kulimwa katika ardhi zisizo na rutuba katika nchi za 'Ukanda Mmoja na Njia Moja'. Hivi sasa nchi nyingi kama vile Pakistan na Myanmar zimeagiza mpunga huo."

    Mjumbe Zhao Wanping pia amesema China na nchi za Afrika zinaweza kuimarisha zaidi ushirikiano wao katika sekta ya kilimo ili kuzisaidia nchi hizo kupambana na umaskini.

    "katika baadhi ya nchi za Afrika, bado kuna watu wanaishi na njaa, na watu wapatao bilioni 1 wanakabiliwa na suala la njaa. Na kufanya ushirikiano wa kilimo na China sio tu kunaweza kuzisaidia nchi hizo kuondokana na tatizo la ukosefu wa mazao ya kilimo, pia kunaweza kutatua tatizo ambalo limesumbua nchi hizo kwa muda mrefu, yaani njaa na kupunguza umaskini."

    Kwa muda mrefu, China na Afrika zimedumisha ushirikiano wa kina katika sekta ya kupunguza umaskini, jambo ambalo limeonesha matarajio mazuri ya watu wa China ya kupenda kubadilishana maoni na watu wa dunia nzima katika kupunguza umaskini. Takwimu zimeonesha kuwa tangu mwaka 2006, wizara ya kilimo ya China pekee imeandaa madarasa 260 na kutoa mafunzo kwa maofisa wa kilimo na wenye ujuzi elfu 5 kutoka nchi 54 za Afrika. China imewekeza dola za kimarekani bilioni 1 katika sekta ya kilimo barani Afrika na makampuni ya China yamewaajiri wafanyakazi wazawa zaidi ya elfu 15 na kuwasaidia wakulima wa Afrika karibu laki moja kujishughulisha na uzalishaji wa kilimo. Vilevile, wataalamu na wenye teknolojia wa China wametekeleza miradi ya kielelezo 300 na kueneza teknolojia aina 450 za kilimo barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako