• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali yatenga dola milioni 200 za kuendeleza mashamba ya mitende

    (GMT+08:00) 2018-03-12 19:24:02

    Serikali ya Uganda imepata dola milioni 200 za kufanikisha mradi wa mitende ya mafuta kwa sehemu nyingine za nchi.

    Waziri wa Kilimo, Vincent Ssempijja, ameyasema hayo wakati wa ziara katika mashamba ya mitende ya Kalangala mwishoni mwa wiki.

    Bw Ssempijja alisema serikali imewataka wanasayansi wa mitende ya mafuta kuchukua sampuli za udongo kwa ajili ya kupima baada ya ziara ya mafanikio ya mradi kwenye kisiwa cha Bugala.

    Sampuli za udongo zilichukuliwa kutoka kwa wilaya za Buvuma, Buikwe, Mukono, Mayuge, Namayingo, Masaka na eneo la Bunyoro .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako