• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Serikali ya Tanzania haitatoa fedha kusaidia benki

  (GMT+08:00) 2018-03-12 19:24:46

  Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuanzia sasa serikali haitatoa fedha kuzisaidia benki zinazosuasua katika kujiendesha kama ilivyozoeleka, hata kama benki husika zina mitaji ya serikali.

  Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB mjini Chato mkoani Geita na kusema kuwa benki ni kama biashara nyingine na hivyo zinapofanya vibaya hata kama utakuwa na mtaji wa serikali lazima zitakufa tu.

  Alitoa wito kwa benki zinazosuasua kujiunga na benki kubwa zilizo imara ili ziweze kuwa na nguvu za kujiendesha na benki kubwa ziwe tayari kuzipokea benki hizo ndogo na kuzikwamua kibiashara kama zimeshindwa kusimama zenyewe. Rais Magufuli alieleza kukerwa na tabia za benki ambazo zinashindwa kujiendesha kibiashara, halafu zinasubiri kusaidiwa na serikali na kisha zinaposaidiwa badala ya kujiinua, zinatumia fedha zilizopewa vibaya.

  Rais Magufuli alitoa wito kwa Benki ya Kuu Tanzania (BOT) kuchukua hatua kwa benki zote ambazo zinashindwa kujiendesha kibiashara na kuongeza kuwa ni heri kuwa na benki chache zenye nguvu kama CRDB zinazohudumiwa wananchi kwa ufanisi kuliko kuwa na utitiri wa benki zinazojikongoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako