• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL): Yanga, Azam, Prisons zapaa kuisogelea Simba

  (GMT+08:00) 2018-03-13 08:35:38
  Mabingwa watetezi Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika ligi kuu ya Vodacoma ya Tanzania Bara baada ya kuibamiza Stand United goli 3-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga sasa imefikisha pointi 46 kwa michezo 21. Nayo Azam FC na Tanzania Prisons FC zilmechupa katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kushinda mechi za ligi zilizochezwa wikiendi iliyopita.

  Klabu ya Azam imechupa hadi nafasi ya tatu wakiwa na alama 44 baada ya kuifunga Mbao FC mabao 2-1. Nayo Prisons FC kutoka mjini Mbeya, wamepanda hadi nafasi ya nne baada ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Morogoro kwenye Uwanja wa Sokoine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako