Katika marekebisho ya katiba ya China yaliyopitishwa na Bunge la Umma la China NPC, fikra ya rais Xi Jinping wa China kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya imewekwa kwenye dibaji.
Wataalamu mbalimbali duniani wanaona marekebisho hayo yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo na amani ya China na dunia.
Mtafiti mwandamizi wa mambo ya Asia na Pasifiki katika Chuo cha taifa cha sayansi cha Azerbaijan Bw. Rafiq Abbasov anaona hii ni hatua muhimu ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya nchi, kuimarisha uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China ambacho kitaongoza wananchi kutafuta njia ya kujiendeleza inayolingana na hali halisi ya China na umaalumu wa China.
Mtaalamu wa Jordan kuhusu mambo ya China Bw. Marwan Sudah anaona marekebisho hayo ni uhakikisho kwa China kudumisha maendeleo chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, rais Xi Jinping akiwa kiini chake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |