• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana mjumbe maalumu wa rais wa Korea Kusini

  (GMT+08:00) 2018-03-13 10:11:38

  Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na mshauri wa usalama wa rais wa Korea Kusini Bw. Chung Eui-yong.

  Rais Xi amemshukuru rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kumtuma mjumbe wake kumwarifu kuhusu ziara zake nchini Korea Kaskazini na Marekani. Amesema kwa sasa hali ya peninsula ya Korea ina fursa muhimu ya kufanya mazungumzo na kupunguza mvutano, na China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuhimiza utatizo wa kisiasa wa suala la peninsula ya Korea.

  Bw. Chung amesema Korea Kusini inaishukuru China kusaidia kuboresha hali ya peninsula ya Korea, na pia inapenda kushirikiana kwa karibu na China ili kudumisha mwelekeo mzuri wa sasa kwenye peninsula hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako