• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sea anemone anazalisha sumu tofauti kufuatia mabadiliko ya mazingira

    (GMT+08:00) 2018-03-13 16:04:52

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Hebrew cha Israel wamegundua kuwa kiumbe cha baharini aina ya sea anemone anabadilisha sumu yake mara kwa mara kufuatia mabadiliko ya mazingira.

    Dr. Yehu Moran wa chuo hiki amesema zamani wanasayansi walifikiri kuwa wanyama hawabadilishi sumu yao, lakini baada ya kutafiti sea anemone, wamegundua kuwa wanyama wanaweza kuzalisha sumu tofauti katika mazingira tofauti.

    Baada ya kutafiti sea anemone, kikundi cha watafiti kinachoongozwa na Dr. Moran kimegundua kuwa, sea anemone anapokuwa mdudu mdogo, anazalisha sumu kali ili kuwafanya samaki wasimle. Akiwa mkubwa na kuanza kuwakamata samaki wadogo, anazalisha sumu nyingine. Katika maisha yake anazalisha sumu mbalimbali kwa mujibu wa mabadiliko ya chakula au mazingira.

    Dr. Moran amesema hii inaonesha kuwa wanyama wanaweza kuzalisha sumu mbalimbali ili kuwafukuza wawindaji na kuendana na mazingira yanayobadilikabadilika.

    Ameongeza kuwa sumu ya wanyama hutumiwa kuzalisha dawa, na sumu mbalimbali zinazozalishwa na sea anemone huenda zinaweza kutumiwa kuzalisha dawa mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako