Utafiti uliofanywa na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Chicago nchini Marekani umeonyesha kuwa, China inashinda vita dhidi ya uchafuzi wa hewa, ikiwa ni baada ya miaka minne ya mapambano.
Utafiti huo umesema uwemo wa uchafuzi katika hewa katika miji ya China umepungua kwa kiwango cha asilimia 32 kuanzia mwaka 2014. Data mpya zilizotolewa na serikali ya China mwezi huu zinaonyesha kuwa, idadi ya siku zilizokuwa na uchafuzi mkubwa mjini Beijing zimepungua na kufikia 23 mwaka jana, ikilinganishwa na 58 mwaka 2013.
Utafiti huo pia umesema China imepunguza uwezo wa uzalishaji wa chuma na chuma cha pya, imefunga machimbo ya makaa ya mawe tangu Baraza la Serikali la China lilipoanzisha kampeni ya kudhibiti uchafuzi wa hewa mwaka 2013.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |