Muswada wa sheria ya usimamizi ya China umewasilishwa bungeni ili kujadiliwa kwa mara ya tatu kwa lengo la kuanzisha mfumo wa usimamizi wenye mamlaka, ufanisi, na ulio chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Sheria hiyo mpya inatarajiwa kutumika kama sheria ya msingi na uongozi dhidi ya ufisadi na kwa ajili ya usimamizi wa taifa. Mjumbe Wang Gang kutoka mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur anayehudhuria mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China anasema,(Sauti 2)
"Muswada wa sheria ya usimamizi umebadilisha maamuzi ya Chama cha Kikomunisti cha China ya kufanya uvumbuzi na kukamilisha mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa taifa kuwa sheria, hatua ambayo imeonesha nia imara ya Chama kujisimamia kwa nidhamu kali na kutovumilia hata kidogo vitendo vya rushwa."
Kwa mujibu wa muswada huo, tume mpya za usimamizi zitaanzishwa katika ngazi ya taifa, mkoa, miji na wilaya. Katika kushughulikia uhalifu wa maofisa wanaotumia vibaya madaraka yao, tume hizo zitatekeleza madaraka yao kwa uhuru bila yaingiliwa na serikali, asasi za kijamii na watu binafsi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |