• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya awaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya chuo kikuu cha China

    (GMT+08:00) 2018-03-14 19:14:23

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefanya hafla ya kuwaaga wanafunzi wa chuo cha Confucius cha Egerton waliopata ufadhili wa masomo ya chuo kikuu nchini China.

    Hafla hiyo ilifanyika ikulu mjini Nairobi na kuhudhuriwa na balozi wa China nchini Kenya Bw. Liu Xianfa. Rais Kenyatta ameshukuru China kwa kutoa mchango mkubwa katika elimu na maendeleo ya Kenya. Amesema ushirikiano kati ya China na Kenya una historia ndefu, na nchi hizo mbili zimekuwa washirika wa kimkakati

    Balozi Liu amesema China itaendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano na Kenya katika kuandaa wataalamu wa kilimo na uhamishaji wa teknolojia. Pia amesema tangu Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Egerton kuanzisha chuo cha kwanza cha Confucius cha kilimo mwaka 2012, pande hizo mbili zimeboresha utaratibu wao wa ushirikiano wa kilimo na kupanua maeneo ya ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako