• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wasindikaji watengeneza maziwa ya unga ili kuziba pengo la uhaba wa maziwa

    (GMT+08:00) 2018-03-14 19:26:30

    Wasindikaji maziwa hivi sasa wanatengeneza maziwa ya unga ili kuziba nakisi ya maziwa kutokana na uhaba wa usambazaji maziwa kutoka kwa wazalishaji.

    Mwenyekiti wa Chama cha wasindikaji maziwa cha Kenya Nixon Sigey amesema kiwango cha maziwa kimeshuka kwa asilimia 30,na kusababisha uhaba katika viwanda.

    Sigey amesema wasindikaji wakuu wa maziwa wana takriban tani 5,000 za maziwa ya unga,ambayo yanatosheleza mahitaji ya nchi kwa muda wa miezi miwili ijayo.

    Sigey ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya maziwa ya New KCC amesema uzalishaji wa maziwa umepungua kwa asilimia 30,hali iliyowafanya kutengeneza maziwa ya unga ili kukidhi mahitaji na kudumisha bei za chini kwa wateja.

    Anasema MAziwa ya unga yamesaidia kudumisha bei za maziwa ambapo pakiti ya nusu lita inauzwa Sh50 kwa wastani ikilinganishwa na bei ya Sh60 kwa kiwango hicho hicho mwaka uliopita.

    Takwimu kutoka Bodi ya Maziwa nchini Kenya (KDB) zinaonyesha kuwa asilimia ya kupungua huko kulikoandikishwa mwezi uliopita ni kubwa sana kuliko ile iliyoshuhudiwa kipindi sawa na hicho mwkaa jana.

    Hata hivyo Mkurugenzi wa KDB Margaret Kibogy alisema wanatarajia kiwango cha maziwa kuongezeka kutokana na mvua zilizoanza kunyesha hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako