• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Baraza la mashauriano ya kisiasa wafungwa

  (GMT+08:00) 2018-03-15 10:40:17

  Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Baraza la mashauriano ya kisiasa la China CPPCC unafungwa mjini Beijing. Viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping wa China wanahudhuria sherehe ya kufungwa kwa baraza hilo.

  Wajumbe wa mkutano huo watapiga kura kuhusu mswada wa uamuzi kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya CPPCC, mswada wa uamuzi kuhusu rasimu ya marekebisho ya katiba ya CPPCC, mswada wa ripoti kuhusu ukaguzi wa mapendekezo, na mswada wa rasimu kuhusu azimio la kisiasa.

  Akihutubia sherehe ya kufunga mkutano huo, mwenyekiti mpya wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Wang Yang amesisitiza kuwa, baraza hilo linatakiwa kutekeleza kwa makini moyo wa Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China, na kuichukulia fikra ya Rais Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalum wa China kwenye zama mpya kuwa mwongozo mkuu wa kazi zote, na kutekeleza majukumu yake kwa makini, ili kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya baraza hilo katika zama mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako