• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Njia mpya ya kupunguza hatari ya ndege kupigwa na radi

  (GMT+08:00) 2018-03-15 16:23:15

  Watalaamu wa safari za ndege wamekadiria kuwa kila ndege ya kibiashara hupigwa na radi mara isiyopungua moja kila mwaka, na asilimia 90 ya matukio hayo yanasababishwa na ndege zenyewe. Watafiti wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachusetts wamesema kutia umeme nje ya ndege kutaweza kupunguza hatari ya kupigwa na radi.

  Wakati ndege inaporuka katika mvua yenye radi, chaji hasi na chanya zinaanza kujaa kwenye pande mbili za ndege. Tofauti ya volteji ya pande mbili ikifikia kiasi fulani, mtiririko wa plasma unaoweza kupitisha umeme unatokea, na kuifanya ndege iwe rahisi zaidi kupigwa na radi.

  Watafiti wamesema watu wakipima chaji zilizoko nje ya ndege, na kuzirekebisha kwa kutia umeme kidogo, watapunguza uwezekano wa ndege kupigwa na radi.

  Majaribio ya mwanzo yanaonesha kuwa baada ya kurekebisha chaji zilizoko nje ya ndege, chaji kiasi tu ikiongezeka kwa asilimia 50, ndege inapigwa na radi. Katika siku zijazo watafiti wataendelea kufanya majaribio ya kurusha ndege isiyo na rubani wakati inanyesha mvua yenye radi.

  Kwa kawaida radi haitahatarisha usalama wa abiria, lakini huenda ikaharibu ndege na vyombo vya umeme, na ndege ikiharibiwa vibaya, haiwezi kutumiwa tena.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako