• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa vyama vingi unaoongozwa na CPC na mfumo wa mashauriano ya kisiasa ni mfumo wa siasa wa kimsingi

    (GMT+08:00) 2018-03-15 16:27:55

    Mkutano wa kwanza wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC umefungwa leo hapa Beijing.

    Akihutubia mkutano huo, mwenyekiti mpya wa CPPCC Wang Yang amesema ushirikiano wa vyama vingi unaoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China na mfumo wa mashauriano ya kisiasa ni mfumo wa siasa wa kimsingi, umesanifiwa na Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa China na vyama mbalimbali vya kidemokrasia, pamoja na watu wasio wanachama, ni mfumo wa vyama vya kisiasa wa aina mpya uliochipuka katika ardhi ya China.

    Bw. Wang amesisitiza kuwa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China linatakiwa kuzingatia umuhimu wa siasa, kuweka kipaumbele kwa maslahi ya wananchi katika kutekeleza majukumu yake na kuinua uwezo wa kufanya mashauriano kwa kuangalia hali halisi na ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako