Kamati ya Usimamizi wa Dhamana ya China (CSRC) imeimarisha ufuatiliaji dhidi ya ukiukaji wa kanuni za soko la fedha kwa lengo la kulinda maslahi ya wawekezaji.
Tangu mwaka jana, Kamati hiyo imetoa adhabu kwa kampuni 339 zilizosajiliwa katika soko la hisa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutawala soko kwa hila na kufanya biashara ya ndani.
Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka jana, Kamati hiyo ilitoza faini ya dola za kimarekani bilioni 1.8 kwa kampuni mbalimbali, ikiwa ni ongezeko la asilimia 74.74 ikilinganishwa na mwaka 2016. Faini hizo zilitolewa kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kutoa taarifa kwa wakati.
Usimamizi huo mkali umeendelea mpaka mwaka huu, ambapo tayari hukumu za makosa 34 zimeshatolewa na Kamati hiyo tangu mwaka huu uanze.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |