• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Mamplaka ya mapato kufuatalia kodi zilizokwepwa

    (GMT+08:00) 2018-03-15 20:51:44

    Akizungumzia maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wanaowabambikia wananchi kodi, Rais Magufuli aliitaka Mamlaka hiyo kujipanga upya na kubuni mbinu nzuri za kukusanya kodi badala ya kuwabudhudhi walipa kodi.

    Alisema baadhi ya wafanyakazi katika mamlaka hiyo si wazuri wanaipaka matope serikali kutokana na kufanya kazi mbaya ya kutotumia mbinu bora za kukusanya kodi kwa wananchi mbalimbali nchini na kuwafanya wananchi waichukie serikali yao kuwa inatoza kodi kubwa. Rais Magufuli alitoa mfano wa kadi ya majengo ambayo alisema aliagiza mamlaka hiyo kutoza kiwango sawa kwa wenye majengo lakini wao wakawa wakipandisha kodi na kutoza kati ya Sh 600,000 hadi milioni moja, kitendo ambacho kinawakera wananchi.

    Alisema kutokana na kutokuwa na mbinu nzuri za kutoza kodi, baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamekuwa wakitafuta mbinu za kukwepa kodi au kutumia ujanja wa kulipa kodi kidogo na hivyo serikali inapata hasara kutokana na kukweka kodi huko. "Baadhi yao wafanyabiashara au wananchi wamekuwa wakikwepa kodi kwa kutoa risiti ambazo hazilinganisha na fedha walizotoa wateja, hivyo mamlaka hiyo inatakuwa kuangalia mbinu bora za ukusaji kodi ili wananchi waone ni wajibu wao kulipa," alisema.

    Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi kutoka Ihumwa na maeneo jirani ndani ya mkoa wa Dodoma alisema, TRA wanatakiwa kusimamia ukusanyaji wa kodi na kutafuta njia nzuri za kukusanya kodi ili wananchi waone kwamba wana wajibu wa kulipa kodi na ndiyo inayowaletea heshima kwa taifa lao. Aliwaagiza viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kwa Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu kuhakikisha wanakaa na kuweka mbinu na utaratibu mzuri wa kukusanya kodi ambao wananchi watakuwa radhi kulipa badala ya utaratibu wa sasa ambao unasababisha wananchi wengine kukwepa kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako