• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura afungiwa soka maisha

    (GMT+08:00) 2018-03-16 09:06:08

    Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura amefungiwa kifungo cha maisha kwa kutojihusisha na mchezo wa soka popote pale baada ya kukutwa na makosa matatu dhidi yake. Hayo yamebainishwa jana na Kamati ya Maadili ya TFF wakati walivyokuwa wanazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya TFF, Jijini Dar es Salaam na kusema wamemfungia kiongozi huyo kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013 baada ya kupatikana na kosa la kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

    Kwa upande mwingine, Kamati ya Maadili ya TFF imesema adhabu hiyo iliyotolewa dhidi ya Michael Wambura imezingatia vigezo na masharti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako