• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inataka shule za chekechea zinazofaa kwa jamii nzima kufikia asilimia zaidi ya 80

    (GMT+08:00) 2018-03-16 16:28:40

    China itachukua hatua za kushughulikia vizuri elimu ya awali na kujitahidi kufanya shule za chekechea zinazofaa jamii nzima zifikie asilimia zaidi ya 80, na kiwango cha kuingia katika shule hizo kifikie asilimia 85.

    Hayo yamesemwa na waziri wa elimu wa China Bw. Chen Baoguo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kando ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la China unaoendelea hapa Beijing.

    Amesema katika miaka mitano iliyopita, elimu ya awali nchini China imeboreshwa kwa kiasi kikubwa na kwamba shule za chekechea zimefikia laki 2.55, na kwamba kiwango cha watoto wanaokwenda shule hizo wanapofikia umri unaofaa kimefikia asilimia 79.6.

    Hata hivyo amesema elimu ya awali nchini China bado inakabiliwa na changamoto kama vile ukosefu wa shule za chekechea zinazofaa jamii nzima, ukosefu wa walimu wa elimu ya awali na ukosefu wa usimamizi wa usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako