• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KPA kuharakisha upakuaji wa makasha bandarini

    (GMT+08:00) 2018-03-16 19:59:53

    Muungano wa wafanyakazi katika bandari ya Mombasa unalenga kupakua makasha 27 kutoka kwa kreni moja kwa saa.Mpango huo unatarajiwa kuimarisha shughuli za kupakua shehena bandarini na vile vile kuifanya bandari kubwa zaidi barani Afrika. Katibu mkuu wa muungano huo Bw Simon Sang amesema wameafikiana mkataba na halmashauri ya bandari nchini Kenya KPA kuanza mikakati hiyo ndani ya miezi kumi ijayo. Sang amesema hilo linawezekana kwa sababu kuna mashirika mengine ambayo tayari yamefaulu kuweza kupakua makasha hata 33 kwa kreni kwa saa moja.Aidha Sang amepongeza mpango wa serikali kuamua kupeleka mizigo kutoka bandari ya Mombasa hadi katika eneo la Nairobi kupitia kwa reli.Amesema mpango huo utahakikisha kazi katika bandari hiyo haiathiriki kivyovyote na kwamba itapunguza misongamano na ajali barabarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako