• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China wapokea hoja 325 na mapendekezo 7,100

    (GMT+08:00) 2018-03-16 20:01:58

    Ofisi ya sekretarieti ya mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China unaoendelea hapa Beijing imepokea hoja 325 na mapendekezo 7,100.

    Hoja hizo zilizotolewa na wajumbe wa Bunge zinahusu utungaji na marekebisho ya sheria kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa taifa, mageuzi ya vyombo vya kiserikali, ujenzi wa mfumo wa uchumi wa kisasa, pamoja na kulinda na kuboresha maisha ya wananchi.

    Mapendekezo yaliyowasilishwa na wajumbe yanahusu zaidi kuhimiza mageuzi katika muundo wa utoaji bidhaa, kuhimiza maendeleo yenye uwiano, kuongeza nguvu za kuondoa umaskini kwa hatua za kulenga. Pia kulinda rasilimali na mazingira ya asili na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, kutekeleza mkakati wa kukuza vijiji, kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuimarisha mageuzi katika sekta ya matibabu na elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako