• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Xi Jinping achaguliwa kuwa rais wa awamu mpya wa China

    (GMT+08:00) 2018-03-17 11:48:20

    Kikao cha tano cha Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la umma la China kilichofanyika leo asubuhi hapa Beijing, kimepiga kura na kumchagua Bw. Xi Jinping kuwa rais wa Jamhuri ya watu wa China na mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China.

    Mkutano huo pia umewachagua Bw. Li Zhanshu kuwa spika wa Bunge la awamu ya 13 la umma la China, na Bw. Wang Qishan kuwa makamu wa rais wa China.

    Sherehe ya kula kiapo cha kikatiba imefanyika baada ya kikao hicho, na hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa China kula kiapo cha kikatiba tangu utaratibu huu uanzishwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako