Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la umma la China uliofanyika leo asubuhi hapa Beijing, umepiga kura na kuamua Bw. Li Keqiang awe waziri mkuu wa Serikali ya China, na kumchagua Bw. Yang Xiaodu kuwa mkuu wa Kamati ya usimamizi ya taifa ya China.
Pia mkutano huo umepitisha uteuzi wa Bw. Xu Qiliang na Bw. Zhang Youxia kuwa manaibu wenyekiti wa Kamati Kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China, kumchagua Bw. Zhou Qiang kuwa mkuu wa Mahakama Kuu ya umma, kumchagua Bw. Zhang Jun kuwa mkuu wa Idara Kuu ya Uendeshaji mashtaka ya umma.
Baada ya ajenda mbalimbali za mkutano kumalizika, Bw. Li Keqiang, Bw. Yang Xiaodu na viongozi wengine kwa mbalimbali wameapa kwa katiba ya nchi.